Umoja wa Mataifa umeipongeza Tanzania kwa kuendelea kutoa hifadhi kwa Wakimbizi kwani kwa sasa zaidi ya Wakimbizi laki tatu kutoka nchi za Burundi na Kongo wanahifadhiwa nchini huku ongezeko la watu kukimbia nchi zao kwa kutafuta hifadhi likitajwa kuendelea kukua kwa kasi.
Akiongea wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mkimbizi Duniani iliyofanyika June 20 yenye kauli mbiu piga hatua na Mkimbizi, Mratibu Mkazi Umoja wa Mataifa Alvaro Rodriguez amesema nchi ya Tanzania inapaswa kupewa pongezi kwa kuendelea kutoa hifadhi kwa Wakimbizi ambapo amesema kwa sasa masuala ya ukimbizi ni janga la kidunia linalohitaji ufumbuzi wa haraka.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amehimiza jamii ya Wakimbizi kutokuvunja Sheria za nchi pamoja na kuwa tayari kurejea nchini kwao kwani hari ni shwari.
TAZAMA WAREMBO WAKIMBIZI WAKISHINDANA U-MISS, WANAUME FASHION