Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya timu ya taifa ya Senegal, ameongea na waandishi wa habari leo akiwa jijini Cairo, Senegal kuelekea mchezo huo watamkosa staa wao Sadio Mane ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano.
Hivyo wengi walijua kuwa kutokana na kukosekana katika mchezo wa kesho kwa Sadio Mane labda Tanzania itapata urahisi, Samatta ameeleza kuwa kukosekana kwa huyo bado hakuifanya Taifa Stars kujiamini kwa asilimia 100 kuwa watashinda kwa sababu Senegal ni timu kongwe na nzuri.
“Tunaamini wao ni timu kubwa Afrika wawe wanacheza na Sadio au bila ya sadio tutashindana nao na kujaribu kuchukua point, nafikiri sio siri timu ya Senegal ni imara na kila mmoj Afrika anafahamu hilo”>>> Samatta
HALI ILIVYO NJE YA UWANJA WA CAIRO INTERNATIONAL KUELEKEA DR CONGO VS UGANDA