Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula amepiga marufuku wananchi wanaoshtakiana katika Mabaraza ya Ardhi kutoa pesa kwa ajili ya kugharimia usafiri wa kwenda eneo lenye mgogoro.
Akizungumza wakati wa kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Dkt. Mabula amesema, kutoa pesa ya kugharamia usafiri kwa mmoja wa wanaoshitakiana katika Mabaraza ya Ardhi kwenda eneo la tukio kunaweza kuleta ushawishi kwa wajumbe wake hasa kwa yule aliyetoa kiasi kikubwa cha pesa.
‘’ Jamaa anatoa laki mbili anayelalamika hana kitu unategemea hapo haki itatendekaje, ni marufuku kabisa na taratibu zote za kwenda uwandani zipitie kwa DC na ratiba ijulikane mapema’’ Dkt. Mabula.
“AKIONA HATUMSAIDII ANATUONDOA, MNIOMBEE NISITOKE MAPEMA” MKURUGENZI TIC