Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa daraja linalokatiza baharini kwa kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini DSM kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
Rais Magufuli ameshuhudia shughuli za ujenzi zikiendelea vizuri ambapo mkandarasi ambaye ni kampuni ya GS Engineering ya Korea anakamilisha kuunganisha daraja la muda litakalomwezesha kuanza ujenzi wa nguzo za daraja. Kwa ujumla kazi imefikia asilimia 10.12.
Akiwa katika mradi huo Rais Magufuli amekutana na Mhandisi Mshauri kutoka kampuni ya Yooshin Engineering Mhandisi Suk-Joo Lee na kumuelezea kufurahishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo linatarajiwa kusaidia kupunguza msongamano wa magari kutoka na kuingia katikati ya Jiji la DSM.
Nae Suk-Joo Lee ameelezea kufurahishwa kwake kufanya kazi Tanzania na ameahidi kuwa kazi hiyo itakwenda vizuri.
.BOSS WA BWANA HARUSI KAFUNGUKA A TO Z ALIVYOFARIKI BI.HARUSI AJALINI, GHARAMA YA HARUSI