Baada ya saa chache kuripotiwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Starehe Charle Kanyi ‘Jaguar’ kukamatwa na Polisi kutokana na kauli yake iliyotafsiriwa kuwa ni ya kibaguzi dhidi ya Raia wasio Wakenya rwanaofanya biashara Nchini humo ameandika kupitia ukuarasa wake wa Instagram.
Mbunge huyo ameandika kuwa kauli yake imetafsiriwa vibaya juu ya masoko ya Wakenya ambapo anadai kuwa alichotaka ni biashara za Wakenya kutobugudhiwa na alimalizia kwa kusema kuwa Raia wote kutoka nchi nyingine wanakaribishwa Kenya.
“Kutokana na kauli yangu iliyopita imeonekana kutafsiriwa tofauti nilichokimaanisha ni kuhusu amani kwenye Nchi yangu na biashara zisiingiliwe, wageni wote wanakaribishwa Nchini kwetu” >>>aliandika Mbunge Jaguar.
VIDEO: UGONJWA ULIVYOMBADILISHA KUWA KAMA ‘NYANI’, HAUTIBIKI