Baada ya kupoteza kwa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa mara ya pili mfululizo katika michezo ya Kundi C, nahodha wao Mbwana Samatta baada ya kupoteza mchezo wa pili dhidi ya Kenya kwa magoli 3-2 aliongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa ni tatizo la timu nzima sio kumlaumu mchezaji mmoja mmoja.
“Tusianze kutoa lawama kwa mmoja mmoja nafikiri ni timu nzima hatukuwa matured enough kuweza kulinda ushindi wetu, sio tatizo la ulinzi ni tatizo la timu nzima na kwenye matokeo kama haya tungeweza kufanya vizuri bado tupo kwenye mashindano kuanguka ni kujifunza, watanzania tumewaangusha sana”>>> Samatta
Timu ya taifa ya Tanzania mchezo wao wa mwisho watacheza July 1 2019 dhidi ya timu ya taifa ya Algeria walio vinara wa Kundi C kwa kuwa na jumla ya point 6, Senegal wakiwa nafasi ya pili kwa kuwa na point tatu tofauti ya magoli dhidi ya Kenya waliopo nafasi ya tatu wakati Tanzania ikiburuza mkia.
VIDEO: Jamaa kawa gumzo Cairo wakiamini ni MO Salah kumbe wamefanana