Timu ya taifa ya Kenya imefanikiwa kupata ushindi wa 3-2 wa Kenya dhidi ya Tanzania katika michuano ya AFCON 2019, ushindi huo kwa mujibu wa mfungaji wa magoli mawili ya Kenya Ogada Olunga anaeleza kuwa inatokana na Tanzania kucheza mchezo wa kujihami kipindi cha pili, hiyo ikapelekea Tanzania kukaribisha presha zaidi langoni kwake.
“Taifa Stars walikuwa wazuri lakini ilifika mahali walikuwa wamechoka na unajua hewa ilikuwa nzito pia walicheza vizuri kwa umoja, nafikiri na walirudi nyuma kujihami zaidi na unajua ukiendelea kujihami sana unakaribisha mashambulizi”>>> Olunga
“Walianza kupaniki nikajua hatuwezi kumaliza nao sawa”- Wanyama