Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe amesema matukio ya utekaji ni Utamaduni mpya unaendelea nchini ambao utaiondolea nchi sifa.
Akizungumza na waandishi wa nje ya Mahakama Kuu, Membe amesema “Huu ni utamaduni mpya ambao haukubaliki na ningependa kuchukua nafasi hii kusema kwamba suala la utekaji na watu kupotea linaweza kuiondolea nchi yetu heshima duniani tangu tupate uhuru, hivyo ningependa kuwaomba viongozi wote walikemee,”
“Viongozi wa serikali wasione aibu hata wa Dini wasiogope na wastaafu wote lazima tukemee utamaduni huu mpya, hatuwezi kuendelea kuishi katika nchi yenye watu wenye wasiwasi na uoga ambao hawajui kesho wataamka vipi na hii ajenda iishe maana isipo isha itaenda kwenye uchaguzi mwakani,” Membe
RC MWANRI KAIBU NA JIPYA “WOTE WAONDOKE MJINI, KAGUA CHUMBA KWA CHUMBA”
KIJANA MTANZANIA ALIEAMUA KUUZA KARANGA KUKUSANYA ADA YA KUSOMEA URUBANI, TAYARI AMESHAPATA MILIONI 9, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA