Baada ya kushiriki kwa fainali za AFCON kwa mara nyingi pasipo wahi kushinda taji hilo katika maisha yao, serikali ya Senegal mwaka huu wanaamini ni zamu yao na ndio maana waliamua kutoa zaidi ya Tsh Bilioni 11 za maandalizi ya michuano hiyo, pamoja na maandalizi yao hayo lakini wengi wao wanaitabiria Ubingwa
Kiungo wa club ya Everton na timu ya taifa ya Senegal Idrissa Gueye baada ya kumalizika kwa game hiyo aliongea na waandishi wa habari na alipoulizwa anazungumziaje kuhusu kutabiriwa makubwa alijibu kwa kifupi tu kuwa subiri tuone.
“Leo tuna furaha kitu muhimu kwetu ilikuwa ni kufuzu hatua inayofuata na tumefurahi tumelifanikisha hilo, ilikuwa game ngumu Uganda ni timu nzuri na wamejilinda vizuri”>>>Idrissa Gueye kiungo wa Everton na Senegal
Baada ya ushindi huo Senegal sasa watacheza dhidi ya Benin katika mchezo wa robo fainali ya michuano hiyo, Benin ambao wamepita kwa njia ya Best Looser kuingia hatua ya 16 bora na baadae kuitoa vigogo Morocco kwa mikwaju ya penati 4-1, hiyo ni baada ya mchezo huo kuchezwa na kumalizika kwa dakika 120 wakiwa sare ya 1-1.
VIDEO: Kinachomfanya Bongo Zozo asite kuomba uraia wa TZ, Maisha yake?