Moja kati ya club kubwa Afrika kwa karne sasa ni pamoja na club ya Al Ahly ya Misri ambayo ilianzishwa tokea mwaka 1907, club hii ya wanachama kama ilivyo kwa club za Simba na Yanga lakini imeweza kumudu kujiendesha kwa viongozi waliopo kuweka mifumo rasmi ya club hiyo kujiingizia kipato na kujiendesha.
Al Ahly imewahi kuthubutu kufanya usajili wa mchezaji mmoja tu kwa kiasi cha Tsh Bilioni 1, kitu ambacho kimekuwa kikiwashangaza wengi na kujiuliza hivi club hii inapata wapi pesa, ukweli ni kwa AyoTV ambayo imeweka kambi Cairo Misri imepata nafasi ya kutembelea miundombinu.
Vyanzo vya mapato vya club hiyo ukiachana na ada za wanachama vinatokana na mauzo ya jezi, migahawa mikubwa iliyopo katika jiji la Cairo lakini club imekuwa na udhamini mkubwa sambamba na kumiliki miundombinu yake ambayo inaipunguzia club gharama zinazoweza kuepukika club ina uwanja, swimming pool, timu ya Volley Ball na Basket Ball. Bonyeza PLAY kutazama baadhi ya miundombinu yao.
VIDEO: Uamuzi wa Sadio Mane baada ya kukosa penati ya pili AFCON 2019