Timu ya taifa ya Misri ambao ndio wenyeji wa AFCON 2019 baada ya kuondolewa katika michuano hiyo hatua ya 16 bora kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Afrika Kusini, Rais wa chama cha soka Misri (EFA) Hani Abou Rida ametangaza kujiuzulu.
Rida amejiulu sambamba na kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo Javier Aguirre aliyekuwa na mkataba hadi 2022, kufuatia kutolewa nje ya michuano hiyo ikiwa ni kinyume na mataraji yao, Rida kwa sasa ambaye ni mjumbe wa CAF na FIFA ametangaza kuendelea na nafasi moja tu ya kamati ya maandalizi ya michuano hiyo hadi pale itakapo malizika.
VIDEO: Kinachomfanya Bongo Zozo asite kuomba uraia wa TZ, Maisha yake?