Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera aliyepo katika benchi la ufundi la timu ya taifa ya Congo DR kama kocha msaidizi, ameongea na AyoTV baada ya timu yake kuondolewa katika fainali za AFCON 2019 dhidi ya Madagascar kwa kufungwa kwa penati 4-2, hiyo ni baada ya sare ya kufungana magoli 2-2.
Zahera ambaye baada ya kutolewa mashindanoni amekiri kuwa anaenda ulaya nyumbani kwake kupumzika kidogo huku akieleza kuwa amewapa mapumziko ya siku 10 wachezaji wake waliopo katika kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki AFCON 2019 na kutolewa, ameweka wazi kuwa licha ya kuwa ana majukumu ya timu ya taifa lakini ameeleza kuwa usajili unaofanyika ni pendekezo lake ila ameambiwa Gadiel Michael anasumbua kusaini.
“Wachezai wote wa Tanzania wale walicheza AFCON nimewapa mapumziko ya siku 10 na mie nilifanya Ligi Kuu mwaka mzima napaswa kwenda Ulaya wiki moja au siku nane kupumzika, wachezaji wote wanasaini ni mimi niliwachagua nilishauriana na viongozi, kuna mchezaji mmoja juzi walinipigia simu baada ya kuniambia kuwa Gadiel anasumbua kusaini”>>>Zahera
VIDEO: Kinachomfanya Bongo Zozo asite kuomba uraia wa TZ, Maisha yake?