Hivi karibuni Mahakama ya Rufani nchini Tanzania imetengua mwenendo wa hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomhukumu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda adhabu ya kifungo cha nje, kutokana na kasoro za kisheria.
Badala yake mahakama hiyo imeamuru Sheikh Ponda arudishwe kizimbani katika mahakama hiyo ya Kisutu, ili kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na wenzake 49 ianze upya kuanzia pale alipohukumiwa adhabu hiyo, kusisitiza kufuatwa kwa misingi na matakwa ya kisheria.
Mara baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, AyoTV na millardayo.com imeweza kuzungumza na Wakili wa Sheikh Issa Ponda ambaye ni Juma Nasoro.