Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa usiku wa July 9 2019 aliendelea na ziara yake ya siku tatu nchini Misri lakini baada ya hapo aliongea na watanzania waishio nchini Misri kwa masomo, biashara na maisha ya kawaida ikiwemo kusikiliza changamoto zao wanazokutana nazo nchini humo.
Pamoja na kukutana nao na kuzungumza nao kwa heshima ya kipekee Waziri Mkuu ameongea na watanzania hao na kuwapongeza kwa kujitokeza uwanjani kuisapoti Tanzania wakati wa michuano ya AFCON 2019, licha ya kuwa haikufanya vizuri katika michezo yake yote mitatu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameahidi kuwa miaka miwili ijayo Tanzania itaenda AFCON 2021 nchini Cameroon kushindana na sio kushiriki.
“Hatua ambayo tumeifikia mwaka huu ya kuingia kwenye makundi kwenye fainali za AFCON kwetu sisi ni msingi mkubwa kabisa, tunaingia kwa mara ya kwanza tunakuja kujifunza tumeona kwa kushiriki na tumejifunza mambo mengi sana na nyine tumeona hamkukata tamaa tuliokwenda kucheza tu mlikuja na mkashangilia sana hongera sana, tunawaahidi michezo mingine ya AFCON miaka miwili ijayo tunakwenda kushindana sio kushiriki”>>>Waziri Mkuu Majaliwa
VIDEO: Kinachomfanya Bongo Zozo asite kuomba uraia wa TZ, Maisha yake?