Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo July 10 2019 atakamilisha ziara yake ya siku tatu nchini Misri, ambapo katika ziara hiyo waziri Mkuu aliongozana na waziri wa kilimo kwa lengo la kuona na kujua fursa mbalimbali zilizopo Misri na kuvutia wafanyabiashara kwenda kuwekeza Tanzania.
Mapema July 9 2019 baada ya kufanya ziara ya kutembelea mfereji mpya wa Suez, Ismailia, Pyramids pamoja na mashamba ya samaki, waziri mkuu aliwaeleza watanzania waishio nchini Misri kuwa Tanzania kwa sasa ni nchi ya pili ikiwa uchumi wake unakuwa kwa kasi baada ya nchi ya Ivory Coast ukiachana na nchi za Misri na Nigeria ambazo uchumi upo juu Afrika.
“Mimi nimekuja Misri lengo hasa la ziara hii nimekuja kuiimarisha mahusiano kati ya nchi ya Misri na Tanzania, nyote mnafahamu nchi hizi mbili kwa miaka mingi toka viongozi walioanzisha nchi zetu awamu ya kwanza ya uongozi Tanzania na awamu ya kwanza ya uongozi Misri walijenga mahusiano, Rais wa kwanza Misri Nasa na baba wa Taifa walijenga mahusiano”>>>Waziri Mkuu Majaliwa
VIDEO: Ahadi ya Waziri Mkuu kwa Watanzania waishio Misri kuhusu Taifa Stars