Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amewataka wananchi nchini wawe na utamaduni wa kushirikiana na Serikali kujenga shule, zahanati, vituo ya polisi katika maeneo wanayoishi kuliko kuwa na akili potofu miradi hiyo inajengwa na Serikali pekee.
Lugola ameyasema hayo wakati akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo, ambapo pia alishirikiana na wananchi wa Kijiji cha Namalebe kushiriki ujenzi wa shule mpya ya msingi ya Ibwagagalilo iliyopo katika Kata ya Chitengule jimboni humo ambayo Serikali imetenga shilingi milioni 96 kwa ajili ya kuikamilisha shule hiyo.
Waziri Kangi Lugola (shule mpya ya msingi) Waziri Lugola pia aliwataka licha ya kuwahamasisha wananchi hao kushiriki matukio ya maendeleo, pia alitoa mabati, saruji, nondo kwa ajili ya ujenzi wa zanahati, na kuongeza madarasa katika shule mbalimbali zilizopo katika jimbo lake.