Takriban watu 12 wameuawa na wengine 30 kujeruhiwa baada ya shambulio la kigaidi lililotekelezwa na kundi la wapinganaji la Al-Shabab katika Hoteli ya Asasey iliyoko pembezoni mwa bandari ya Kismayo nchini Somalia.
Maafisa na wale walionusurika wanasema kuwa mlipuaji wa kujitolea muhanga aliligongesha gari lililojaa vilipuzi katika hoteli hiyo kabla ya washambuliaji hao kuvamia jengo hilo.
Kundi la wapinganaji la Al-Shabab limekiri kutekeleza shambulio hilo.
Walioshuhudia wanasema kuwa walisikia milio ya risasi baada ya bomu lililokuwa ndani ya gari hilo kulipuka.