Watu watatu wakazi wa Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwemo kuiba madini yenye thamani ya Sh. Mil 507,347,000.
Washtakiwa hao ni Donald Njonjo (30) Mkazi wa Kigamboni, Gamba Muyemba (51) Mkazi wa Tandika na Kashif Mohamed (41) Mkazi wa Upanga jijini Dar es Salaam ambao wanadaiwa kuiba madini kwenye Tume ya Madini.
Kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa kati ya Novemba 30, 2017 na Juni 29, mwaka huu katika Ofisi ya Tume ya Madini iliyopo Masaki wilayani Kinondoni, waliiba madini ya dhahabu yenye uzito wa Kilogramu 6.244 yenye thamani ya Sh.Mil 507,347,000 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, kesi imeahirishwa hadi Julai 29, 2019 kwa ajili kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuwapatia dhamana.
HATARI: ‘SI BINADAMU WA KAWAIDA’ ANAKULA CHUPA NZIMA, VIWEMBE KAMA BISCUTS