Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli amemtaka Simbachawene kuhakikisha fedha nyingi zinazoelekezwa katika masuala ya mazingira zinaleta matokeo ya kuboresha mazingira, vibali vya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) haviwi kikwazo cha uwekezaji na kutekeleza maagizo yanayotolewa na Serikali kwa wakati.
“Nakumbuka suala la mifuko ya plastiki limechukua muda mrefu, karibu miaka minne, nimetia saini halikutekelezwa, Makamu wa Rais akazungumza weee halikutekelezwa, Waziri Mkuu akazungumza Bungeni halikutekelezwa, mpaka mwishoni mwishoni hapa nilipotoa amri ya lazima ndipo likaanza kutekelezwa, sasa usiende kufanya hivyo wewe (Simbachawene)” Rais Magufuli.