Leo July 23, 2019 Boris Johnson amechaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama cha Conservative katika kura iliyopigwa na wanachama na atakuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza.
Amemshinda mpinzani wake Jeremy Hunt kwa kura 92,153 dhidi ya 46,656.
Meya huyo wa zamani wa mji wa Londona anapokea wadhifa huo kutoka kwa Theresa May kesho Jumatano.
Katika hotuba yake baada ya ushindi huo, Johnson ameahidi kuwa “ataiwasilisha Brexit, kuiunganisha nchi na kumshinda Jeremy Corbyn”.
Akizungumza mjini London, alisema “Tutaipa nchi nguvu.
“Tutaiwasilisha Brexit kufikia Oktoba 31 na kuchukua fursa zote zitakazotokana na muamko mpya wa inawezekana”
“Tutajiamini upya na tutainuka upya na kuondosha shaka na fikra za kutojiamini.”
Bi May amempongeza Johnson, na kumauhidi “ushirikiano wake kikamilifu kutoka nafasi ya nyuma”.