Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dr Harisson Mwakyembe leo ametangaza rasmi kuunda kamati ya usimamizi wa kanuni chini ya BMT ya kueleza kuwa hakuna mtu binafsi atakayeruhusiwa kumiliki asilimia 49 ya hisa katika klabu za wanachama zaidi itaruhusiwa wawe zaidi ya watu watatu na kuendelea ndio waweze kumiliki hisa hizo.
Hivyo wataunda kamati maalum ya kufanya mabadiliko madogo ya kanuni ila kama kuna mtu atataka kumiliki asilimia 49 pekeake katika klabu za wanachama basi atashauri aanzishe timu yake binafsi ili kuweza kuwa na humiliki kamili wa timu.
Baada ya kauli hiyo kutolewa leo mbele ya waandishi wa habari, wengi wamedai kuuliza nini mstakabali wa Simba SC na muwekezaji wao Mohammed Dewji ambaye awali aliripotiwa kushinda zabuni ya uwekezaji ndani ya Simba SC kwa Tsh Bilioni 20 na atakuwa akimiliki asilimia 49.
VIDEO: “Narudia tena Yanga na Simba Sio wenye CECAFA”-Musonye