Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mbugani mwenye umri wa miaka 14, amedai kufanyiwa ukatili kwa kubakwa na wanafunzi watatu ambao wawili wanasoma kwenye Shule ya Sekondari ya Nyanza na mmoja Shule ya Sekondari ya Geita na wote wapo kidato cha pili umri wao ni kati ya miaka 14-15.
Akizungumza na AyoTV kwenye ofisi za Serikali ya Mtaa wa Msalala road Mjini Geita ,Mwanafunzi ambaye amefanyiwa tukio hilo, amesema kuwa wanafunzi hao walikuja shuleni kwao wakati wa mapumziko na kumtaka awasindikize nyumbani ndipo walipofika kwenye chumba wanachoishi na kumsukuma ndani kisha kumziba mdomo na kuanza kumbaka mmoja baada ya Mwingine.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo nakusema kati ya watuhumiwa watatu mmoja ndiye anashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi na pindi upelelezi utakapokamilika jarada litafikishwa kwa mwanasheria mkuu wa Serikali kwa ajili ya hatua za kimahakama.