Serikali ya Tanzania kupitia kwa Msemaji Mkuu wake Dkt Hassan Abbasi imetoa ufafanuzi kuhusu ndege ya ATCL kuzuiliwa Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama Kuu Nchini humo, huku ikibainisha kuwa chanzo ni Kesi ya madai ya muda mrefu ya fidia ya ardhi iliyotwaliwa tangu miaka ya 1980 ikimuhusisha Hermanus Steyn na Serikali ya Tanzania na kwamba kesi hiyo haina uhusiano wowote na Shirika la Ndege la ATCL na Shirika hilo halidaiwi.
“Kwenye awamu zote kulikuwa na makubaliano lakini ukifuatilia hatua za Kimahakama wanakubaliana lakini malipo hayafanyiki, kiasi kikubwa cha malipo kilifanyika katika awamu ya nne kikabaki kiasi kidogo ambacho ndio unaona amekwenda Afrika Kusini” – MSEMAJI MKUU WA SERIKALI