Godfrey Nasary ni mkazi wa Kijiji cha Tindigani Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro amesema amekuwa akirushiwa mawe kwa zaidi ya siku 20 bila kumuona anayerusha mawe hayo huku yakiharibu nyumba yake ikiwemo mabati pamoja na vioo.
Anasema wakati akiwa na Wachungaji wanaomba wanashangaa mawe yanarushwa na kuna siku jiwe lilirushwa likiwa linawaka moto huku akihusisha suala hilo na mambo ya kishirikina.