Jumatano ya March 26 2014 kulikua kufanyike mjadala wa wajumbe wa bunge la katiba Dodoma kuijadili hotuba ya Rais JAKAYA KIKWETE aliyoitoa wakati wa kuzindua bunge maalum la katiba pamoja na ile ya rasimu ya katiba iliyowasilishwa na mwenyekiti wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba lakini mjadala huo umesitishwa.
Maombi ya kujadiliwa kwa rasimu na hotuba hiyo yalitolewa na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo waliodai kuwa hotuba ya Rais inakinzana na rasimu ya katiba.
Akitangaza uamuzi huo mwenyekiti wa bunge Samwel Sitta amesema amepokea maoni kutoka sehemu mbalimbali na kamati ya uongozi kwamba kuruhusu mjadala huo ni sawa na kuwaisha shughuli za bunge kabla ya wakati wake ambapo sababu nyingine za kusitishwa ni za kikanuni.
Namkariri Samwel Sitta akisema >>> ‘kwa msingi huo hakutakua na mjadala wowote kuhusu zile hotuba mbili, nawaomba waheshimiwa msichukue kwamba maudhui yoyote yaliyomo kwenye hotuba zile ni sehemu ya kujiimarisha katika kuzungumzia rasimu yetu ya katiba ambayo ndio kazi ya msingi tuliyokabidhiwa’
Katika sentensi nyingine umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) umeeleza kutokubali mjadala wowote wa mabadiliko ya kanuni kabla ya kutolewa kwa maamuzi ya upigaji wa kura ya siri au ya wazi yaliyopo kwenye Vifungu vya 37 na 38 vya kanuni za Bunge kama wanavyoeleza TUNDU LISSU na JAMES MBATIA.
Tundu Lissu >>> ‘hakuna kufungua mjadala wa kanuni isipokua kile kiporo cha kanuni ya 37 & 38 zinazohusu kura ya wazi au kura ya siri, utaratibu wa kupiga kura kwa Elektroniki sio utaratibu wa siri’
James Mbatia >>> ‘Sasa kama tulikubaliana kwa pamoja kwamba kanuni ni hizi hapa, huyo wa mwenye mambo mengine tofauti na maridhiano yetu ametoka wapi? kwa madaraka yapi? kwa ujanja gani? hatutokubali’
Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA FREEMAN MBOWE na Prof. IBRAHIM LIPUMBA wa chama cha wananchi CUF wameahidi kupambana kusimamia haki ili kuhakikisha Tanzania inapata Katiba Bora itakayofaa kwa sasa na kwa vizazi vijavyo.
>>> ‘Tumefanya uvumilivu mkubwa sana mpaka sasa hivi, hatuondoki hapa mpaka tunahakikisha hii rasimu ya Wananchi inajadiliwa na bunge maalum’