Spika wa Bunge, Job Ndugai ametangaza kuwa kuanzia kesho, Bunge halitagawa karatasi hizo kwa Wabunge ikiwa ni moja ya hatua ya kuondokana na matumizi ya karatasi.
Ndugai ametoa kauli hiyo leo, wakati akitoa matangazo mbalimbali kwa Wabunge na kubainisha kuwa badala yake watatumia simu zao na barua pepe.
“Hizi karatasi za pinki hii ndo itakuwa ya mwisho kuingia Bungeni leo. Kuanzia kesho tutatumia mawasiliano yako ya kimtandao, kila mmoja ahakiki namba yake ya WhatsApp na Email.” Spika Ndugai
Amesema Bunge la Tanzania ndo Bunge pekee Afrika Mashariki linaloendeleza matumizi ya karatasi “Wenzetu wote ni ‘paper less’ hivyo tutaanza na hii kwanza.”.