Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji nchini Tanzania, Thobias Andengenye amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji.
Taarifa iliyotolewa leo Septemba 3, 2019 na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Joseph Mwasabeja imesema katika mabadiliko hayo aliyekuwa kamanda wa Jeshi la polisi na uokoaji mkoa wa Morogoro, Gilbert Mvungi amehamishiwa makao makuu ya zimamoto na uokoaji Dodoma.