Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi wilayani Same Mkoani Kilimanjaro Dr Mathayo D. Mathayo ametenga Zaidi ya Tsh million 100 kwa ajili ya kuibua vipaji na kuimarisha michezo katika jimbo hilo.
Mbunge huyo ambae ameanza kugawa mipira katika kila kata kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao yatashindanisha timu za wanawake kwa upande wa mpira wa pete na wanaume kwa upande wa mpira wa miguu.
Akizungumza na wananchi wa kata zote 20 anazotembelea Mathayo amesema katika kila kata watashindana vijiji kwa vijiji kwa mtindo wa marudiano mara tatu tatu ili aweze kupatikana mshindi kwa upande wa wanawake na wanaume.
“Nataka mshindane kila kijiji na kijiji na kijiji kitakachoshinda kwenye kila kata, kitapata zawadi ya shilingi milioni mbili kwa timu ya wanawake na shilingi milioni mbili kwa timu ya wanaume”>>> Mathayo
Mathayo amesema ametenga Tsh milioni 80 kwa ajili ya timu zitakazoibuka kidedea katika kila kata, Mathayo pia amekuwa akigawa mipira katika shule za msingi na sekondari katika kata mbalimbali jimboni kwake.
“Ndugu zangu michezo ni afya michezo ni ajira leo namkabidhi mhe diwani hii mpira lakini asiigawe mpaka nitakapoleta jezi ili muanze mashindano hayo mkiwa na jezi zinazotofautina au mnataka kucheza kienyeji”>>> Mathayo