Moja ya Wachungaji waliopata nafasi ya kuzungumza mbele ya Rais Magufuli leo September 4, 2019 ni Mchungaji Daniel Mgogo ambapo amewaacha watu hoi kwa vicheko ukumbini wakati akieleza juu ya Ukandarasi ndio ilikuwa moja vitu vya awali MUNGU kufanya.
“Tumewasomesha mmesoma, mtusaidie Sisi tuliokimbia umande, mnatuuzia Viwanja ambavyo vipo barabarani, tunawaomba na nyie mtujengee mnapima tu! bila kutuambia, Sisi ambao hatuna elimu hiyo, Watoto wa Mjini wajanja” – Mch. Daniel Mgogo Mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.