Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, amemualika Bungeni Mbunge aliyekaa kwa muda mrefu jimboni kwa miaka 45, Chrisant Mzindakaya na kuwataka Wabunge wote waige mfano wake.
“Leo nimemualika maalum hasa kwa Wabunge vijana muweze kumfahamu huyu alikuwa Mbunge kwa miaka 45 mfululizo, hii ni rekodi ambayo hamuwezi kuifikia hata mtambike, alianza 1945 hadi 2010“ Ndugai.
“Mzindakaya amepata tuzo mbalimbali za utumishi ikiwemo tuzo ya Mwalimu Nyerere, tuzo kutoka Umoja wa Vijana, aliandikiwa barua na Rais Mwinyi ya kupongezwa kwa utendaji kazi wake, naomba mfuate nyayo zake“ Ndugai.