Itakumbukwa Siku chache zilizopita @ayotv_ na millardayo.com tulitoa taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro kuanzisha oparesheni ya kusitisha vitendo vya Wazazi kuwapeleka unyago Watoto wao wa kike wenye miaka 5 hadi 14, huku akidai anasitisha vitendo hivyo kwakuwa Watoto wanafundishwa mambo ya kikubwa na kuwafanya washindwe kumudu vema masomo yao huku wakichochewa kuanza ngono wakiwa wadogo na hata kupelekea kushamiri kwa mimba za utotoni.
Sasa Founder wa Taasisi ya kupigania haki za Watoto, Vijana na Wanawake ya TUPAZE SAUTI FOUNDATION, Agness Kahamba amefunga safari hadi Tunduru kujionea hali halisi “Kule Tunduru kuna mila fulani imewekwa, Binti akifikisha miaka 14 anapelekwa unyago na wakiwa uko wanafundishwa vitu vya kikubwa, kwahiyo wakitoka wanawaza nimpate mwanaume mwenye hela nimfanyie vile vitu nilivyofundishwa, kwa mwezi wa nane pekee Wanafunzi 23 wa Form IV wamegundulika kuwa na mimba “