Shirikisho la soka Tanzania TFF leo limetangaza kuingia mkataba wa miaka minne na kampuni ya Azam TV kwa ajili ya kuonesha michuano ya Kombe la FA (Azam Sports Federation Cup) pamoja na michezo ya kirafiki ya timu za taifa isiyokuwa na hakimiliki na CAF na FIFA.
Mkataba wa TFF na Azam Media wa miaka 4 na una thamani ya Tsh Bilioni 4.5 lakini wakuonesha mechi za Taifa Stars za kirafiki ni Tsh milioni 400 sawa na Tsh milioni 100 kwa kila mwaka, kwa upande wa Taifa Stars kila itakapokuwa inacheza mechi za kirafiki itakuwa inapewa Tsh milioni 35.
Mkataba wa TFF na Azam Media umesainiwa na Rais wa TFF Wallace Karia mbele ya katibu mkuu wa shirikisho hilo pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Azam Media Tido Muhando akiwa pamoja na mkurugenzi wa michezo wa Azam TV Patrick Kahemele.
EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE