Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Yuda Ruwa’ichi, hali yake imeendelea kuimarika na sasa amehamishiwa katika wodi ya kawaida kutoka katika chumba cha ICU.
Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo, Profesa Joseph Kahamba baada ya kutolewa mashine iliyokuwa inamsadia kupumua askofu Ruwa’ichi amekuwa akiendelea vizuri na kufanya mazoezi.
Askofu Ruwa’ichi alifikishwa katika Taasisi ya Mifupa ya Hospitali ya Muhimbili (Moi) akitokea katika Hospitali ya Rufaa Kilimanjaro (KCMC) Jumatatu Septemba 9 na kufanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo.