Viongozi 9 wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe wameshindwa kuanza kujitetea katika kesi ya uchochezi inayowakabili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu mawakili wanaowatetea wanasimamia kesi Mahakama Kuu ya Tanzania.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 24 na 27, mwaka huu. Leo viongozi hao 9 walitarajia kuanza kujitetea baada ya Mahakama hiyo kuwakuta na kesi ya kujibu kutokana na ushahidi wa mashahidi 8 uliofungwa na Upande wa Mashitaka.