Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma limewakamata watuhumiwa wa uhalifu wanaosafirisha mafuta ya petrol na diesel kwa njia hatarishi kwenye magari ya abiria ambapo jumla ya magari matano yamekamatwa pamoja na watuhumiwa tisa kushikiliwa kwa kutenda makossa hayo.
Kamanda wa Polisi Gilles Muroto amesema hadi sasa jumla ya lita 1277 za Petrol na lita 850 za Diesel zimekwishakamatwa huku watuhumiwa wakisubiri kupelekwa Mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka yao.
BASHUNGWA ATINGA BRELA NA KERO ZA WANANCHI, MKURUGENZI AMJIBU “HATUPOKEI HELA”