Timu ya Ndanda Fc kutoka Mtwara imekuwa timu ya pili kukata tiketi ya kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao baada ya Jumatatu ya March 24 kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Dar mechi iliyochezwa Uwanja wa Karume 88.5 Dar es Salaam.
Ndanda imepata nafasi hiyo baada ya kuongoza Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza ikiwa na pointi 28 na kufuatiwa na African Lyon yenye pointi 27 na Jumatatu March 24 Lyon ilitoka sare ya bao 1-1 na Green Warriors.
Kwa hatua hiyo Ndanda inakuwa timu ya kwanza kutoka Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kucheza Ligi Kuu Bara ambapo awali timu ya Bandari Mtwara ya Mtwara Mjini ndiyo ilikuwa timu ya mwisho kucheza ligi kuu mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Hizi ni picha za mapokezi hayo yaliyoanzia uwanja wa Ndege wa Mtwara kisha kuelekea uwanja wa Nangwanda Sijaona na ratiba itakamilika baadaye kwa kupata chakula cha jioni kwenye ukumbi wa Makonde Beach.