Upande wa Utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa CHADEMA, umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuahirisha kesi hiyo ili wapate muda wa kujiandaa na utetezi.
Hayo yamebainishwa mahakamani hapo na Wakili wa Utetezi, Profesa Abdalah
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa kuanza kujitetea.