Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmauel Maganga amempa masaa 12 Afisa Biashara Wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Elijah Simfukwe kurudisha Tsh.Million Saba na Elfu 40 alizokusanya kutoka katika mauzo ya vitambulisho vya wajasiriamali ambazo hajaziwasilisha Serikalini kwa zaidi ya miezi 3.
Maganga ametoa agizo hilo katika kikao na Watumishi wa Serikali wa Wilaya ya Kigoma baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ugawaji wa vitambulisho vya Taifa na kuelezwa kuwa zaidi ya Tsh.Million saba bado zipo mikononi mwa mkusanyaji.
https://youtu.be/buJqw7erPzs
FAMILIA INALALA NA NYOKA 14 WAKALI WENYE MENO, MTOTO ANAWAOGESHA “BORA JOKA KULIKO MWANANGU”