Jeshi la Polisi wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro leo limezingira mkutano wa ndani wa viongozi wa Chama Cha Demokransia na maendeleo (CHADEMA) uliokuwa ukiongozwa na Mbunge wa jimbo hilo, Freeman Mbowe.
Mkuu wa Wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya amethibitisha kutuma polisi hao akidai lengo ni kuhakikisha usalama wa Mbowe na wananchi kwa ujumla.