Bodi ya Wadhamini ya Chama cha ACT Wazalendo imewasilisha maombi Mahakama Kuu ya Tanzania kutaka waunganishwe katika kesi iliyofunguliwa na Mkulima Patrick Dezydelius Mgoya kuhusu ukomo wa urais.
Kabla ya ACT Wazalendo kuwasilisha maombi hayo kupitia Wakili Jebrah Kambole mbele ya Jaji Elieza Feleshi, tayari Serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, (AG) ilimwekea kigingi mkulima huyo.
Akizungumza na AyoTV, Wakili Kambole amesema kuwa wanaruhusiwa kisheria kujiunga kwenye kesi yoyote ambayo wanaona wanamaslahi nayo, hivyo wanasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu maombi yao.
Mahakama Kuu inatarajia kutoa uamuzi Oktoba 25, 2019 kuhusu maombi ya ACT Wazalendo.