Rais John Magufuli amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kwa kuwachapa viboko wanafunzi wa kidato cha tano na sita wa Shule ya Sekondari Kiwanja wilayani Chunya kwa madai ya kuhusika kuchoma moto mabweni mawili ya shule hiyo.
“Leo nimeongea na Mkuu wa mkoa wa Mbeya na kumpongeza kwa kuwachapa wale wanafunzi viboko, yaani serikali inatoa fedha inajenga madarasa halafu hao wanafunzi wanayachoma, nimeagiza wale wanafunzi kidato cha tano na sita wote wafukuzwe na bodi ya shule ivunjwe” Rais Magufuli