Milvik Tanzania kwa kushirikiana na Tigo Pesa, Resolution na Mo wameshinda tuzo ya Huduma ya Bima Yenye Ubunifu Zaidi kupitia huduma yake ya Bima Mkononi
Alhamisi Tarehe 26 Septemba, 2019 ilikuwa siku muhimu kwa wadau wa bima nchini Tanzania. Kwa mara ya kwanza, wadau wa bima wakiongozwa na TIRA, walitambua michango ya makampuni mbali mbali katika sekta ya bima. Hafla ya kwanza ya kutambua mchango wa makampuni hayo ilifanyika mkoani Mwanza katika hafla ya tuzo za bima yaani 2019 Tanzania Annual Insurance Awards (TAIA).
Milvik Tanzania ilipata tuzo ya Huduma ya Bima yenye Ubunifu Zaidi kupitia huduma yake ya Bima Mkononi, inayopatikana kwa watumiaji wa Tigo Pesa nchini Tanzania. Kamati ya maandalizi ilisema kwamba “Huduma ya Bima Mkononi kutoka Milvik ilionyesha ubunifu wa hali ya juu na pia ushuhuda kutoka kwa watumiaji wake ulidhihirisha kuwa ni ya gharama nafuu na rahisi kutumia. Matumizi ya Tigo Pesa kama mshirika katika kutoa huduma hiyo yanasaidia kurahisisha mchakato wa malipo”.
Berengere Lavisse, Meneja Mkuu wa Milvik alisema “Tunajivunia kutoa huduma rahisi na nafuu kwa wateja wa kipato cha chini kwa ushirikiano na Tigo Pesa, Resolution na Mo.”
“Kupitia bima yetu mpya ya Kulazwa na Watoto, wazazi wanaweza kuwalinda watoto wao kwa matibabu ya kulazwa kwa TSH 750 tu kwa mwezi kwa kila mtoto, kwa kutumia simu zao, bila kujaza fomu za makaratasi na kwa mfumo rahisi wa malipo kupitia Tigo Pesa”.
“Tunawashukuru wateja wetu ambao wameendelea kutuamini katika kulinda hatima za familia zao na tunatarajia kuwaletea huduma zenye ubunifu zaidi katika mwaka 2020.”
WAZIRI MKUU AWAPA MAAGIZO TAKUKURU “FUATILIA KWA KINA WATUMISHI 48 UPOTEVU WA FEDHA”