Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40 hatimae taifa la Iran limeruhusu wanawak kuingia uwanjani kuangalia game za mpira wa miguu toka pale walipokataza rasmi 1979.
Iran ilikuwa ni kosa kwa mwanamke kwenda uwanjani kuangalia mpira toka pale Islamic Revolution walipoa hivyo, licha ya mashirika ya haki za binadamu na FIFA kushinikiza kuruhusiwa huko.
Katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kati ya Iran waliokuwa nyumbani dhidi ya Cambodia, wanawake waliruhusiwa kuingia uwanjani na inadaiwa tiketi zaidi ya 4000 zilinunuliwa na wanawake ambao walishuhudia taifa lao likipata ushindi wa 14-0.