Polisi waliokuwa wakifanya Doria kwenye barabara kuu ya Nairobi-Mombasa Oktoba 15, wamekamata basi la Kanisa la PEFA likiwa na Misokoto 230 ya bangi iliyokuwa imesundwa kwenye eneo la mizigo.
Kulingana na ripoti ya Polisi, basi hilo lilikuwa limesafirisha waombolezaji kutoka Kilifi kwenda Homa Bay na wakati wa kurudi likapakiwa na bangi hiyo.
Tayari dereva wa basi hilo pamoja na watu wengine wawili wametiwa mbaroni ili kusaidia Polisi kwenye uchunguzi wa kisa hicho.
Bangi hiyo inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni 1.