Watendaji Wakuu ambao ni Makatibu Wakuu wa Nchi za SADC katika Sekta ya Mazingira, Maliasili na Utalii wamekutana Arusha kwa ajili ya kuandaa ajenda mbalimbali za Kikao cha Mawaziri wa nchi wanachama wanaohusika na Sekta hizo ambacho kinatarajiwa kufanyika Oktoba 25.