Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Emmanuel Amunike baada ya kupoteza ajira yake ya kuifundisha Taifa Stars mara baada ya AFCON 2019 kumalizika.
Sasa hana timu na katika mahojiano yake na BBC ameweka wazi kuwa anatafuta timu ya kuifundisha kwa sasa, Amunike alipoteza ajira yake July 8 2019 baada ya kushindwa kupata point hata moja katika michezo ya Makundi ya AFCON 2019.
“Niko tayari kuchukua nafasi yoyote itakayotokea kwasababu wiki chache zilizopita nimejifunza mawazo mapya na njia ya kufikia mawazo hayo,” >>> Amuneke
“Kama meneja unahitaji kuwa mkweli na nafasi yako japo Tanzania ukurasa niliufunga, nilijifunza mengi katika kazi hiyo”>>> Amunike
Amunike aliyefutwa kazi aliisaidia Tanzania kufuzu michuano ya AFCON 2019 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 (1980), Amunike aliyepewa kazi ya kuinoa Stars April 2018.