Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amebatilisha pendekezo la kufutwa shamba lenye ukubwa wa ekari 1,000 lililopo Kidunda Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro linalomilikiwa na Rusimbi.
Uamuzi wa Dkt. Mafuli kubatilisha shamba hilo unatokana na kubainika kuwa pendekezo lililowasilishwa la kufutwa shamba hilo kwa madai ya kutoendelezwa kutokuwa za kweli na ulilenga kumdhulumu mmiliki wake.
Akitangaza uamuzi huo wa Rais, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema, baada ya kufuatilia mashamba yaliyopendekezwa kufutwa Dkt. Magufuli alibaini taarifa alizopelekewa za kufuta shamba Cecilia hazikuwa sahihi na hivyo kuamua kubatilisha pendekezo lililowasilishwa kwake na kumpatia haki yake mmiliki.
RC MBEYA “WANAOPINGA MAMBO TUTAWACHAPA VIBOKO, WANAPIGA MANENO YA KIPUMBAVU”