Aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake wawili wanatarajia kuanza kujitetea Novemba 20, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mbali na Aveva wengine ni aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo Godfrey Nyange (Kaburu) pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zachariah Hans Pope.
Wakili wa Serikali, Silvia Mitanto aliieleza mahakama hiyo kuwa wanaomba tarehe ya kutajwa ili weweze kuendelea na rufaa waliokata katika Mahakama Kuu ya Tanzania ya kupinga maamuzi yaliyotolewa na mahakama hiyo kuwaondolea mashtaka ya utakatishaji wa fedha washtakiwa Aveva na Nyange.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema Upande wa Mashtaka kama umekata rufaa utaendelea lakini mahakama hiyo itaendelea na usikilizwaji wa utetezi.
MIFUKO MBADALA FEKI YATEKETEZWA NA NEMC, “HII NI VITA YA UHUJUMU UCHUMI”