Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla akizindua Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Ufugaji nyuki nchini ametoa miezi tatu kwa TANAPA, TAWA na TFS kila Mamlaka kutengeneza mizinga ya nyuki 6000 na kuitundika katika jamii zilizokaribu na Hifadhi ili kujikinga na wanyama hatarishi.
Dkt. Kigwangalla pia amekabidhi mizinga 500 kwa Chuo cha Nyuki Tabora na 500 kwa Chama cha Ushirika cha IPOLE ambapo amesema “kama mfugaji mmoja kapata Milioni nne hawezi kuwa masikini hii ni aina ya uchumi tunaotakiwa kujenga huwa nashindwa kuwaelewa na maPHD yenu”.