Taasisi ya wanawake walioko katika sekta ya bahari Kusini mwa bara la Afrika (WOMESA), tawi la Tanzania leo wamesherehekea maadhimisho ya miaka nane ya taasisi hiyo Unguja Zanzibar.
Katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa kamisheni ya utalii Zanzibar, Sabah Ally amewataka wadau wote wa sekta ya bahari nchini ikiwemo serikali na vyombo binafsi kufatilia kwa karibu changamoto zilizopo na kuzitatua.
Changamoto nyingine zinazoikabili WOMESA ni pamoja na ukosefu wa pesa kuendeshea shughuli zake na ukosefu wa ofisi.
WOMESA ina jumla ya mwanachama 139 kwa sasa nchi nzima ambao ni mabaharia wa kike wakiwemo wahandisi,maafisa na wafanyakazi wengine katika sekta hiyo.